Hakuna kitu chochote kitamu chenye harufu na radha nzuri kama keki uliyoipika kwa mikono yako. Upishi wa keki ni mwepesi sana endapo mpishi atazingatia vitu muhimu vinavyohitajika pamoja na hatua zake.
MAHITAJI
*unga vikombe2
*maziwa kikombe1
*sukari kikombe1
*siagi kikombe1
*baking powder vijiko vidogo 2
*mayai 6 yakienyeji
*vanilla matone mawili au limao 1 Zingatia Limao au vanilla hutumika kwaajili ya kupunguza harufu ya mayai kwenye keki.kwahiyo ukikosa vanilla pia waweza kutumia maganda ya limao. Pia andaa jiko lako la mkaa mapema ili lipate joto pamoja na sufuria iliyopakwa siagi ndani ili kuzuia keki kuganda.
HATUA
*Andaa bakuli lako la udongo na mwiko ambao utatumia kuchanganya mchanganyiko wako
*chukua kikombe kimoja cha siagi na utie katika bakuli pamoja na kikombe kimoja cha sukari.
*koroga mchanganyiko wa sukari na siagi mpaka pale utakapolainika na chembe chembe za sukari kupotea kabisa
*Weka yai moja baada ya jingine huku ukiendelea kuukoroga mchanganyiko wako bila kupumzisha mkono
*Weka matone mawili ya vanilla au maganda ya limao huku ukiendelea kuchanganya.
*Weka unga vikombe viwili uliochanganywa na baking powder kwenye mchanganyiko wako na endelea kuukoroga taratibu
*Baada yahapo tia maziwa kikombe kimoja nauchanganye taratibu
*Mimina taratibu mchanganyiko wako kwenye sufuria maalumu yakupikia iliyopakwa siagi. Zingatia Iwapo utapenda keki yako iwe na rangi unaweza ukaweka kokoa kwenye mchanganyiko wako.
*Weka sufuria ya mchanganyiko katika jiko lenye joto la wastani kwa muda wa nusu saa
*Baada ya hapo toa keki yako tayari kwakuliwa.
Makala hii imeandaliwa na Sara Mourice
Asante Sana
ReplyDeleteNimeipenca post yako. Umeelezea vizuri. Kuna MAPISHI YA KEKI YA MAZIWA unaweza pata maelezo Yale hapo https://www.bongolives.com/2019/04/mapishi-ya-kupika-keki-ya-maziwa.html
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
DeleteAsante..umeelezea vizuri sana na nmeelewa..shukrani
ReplyDeleteHasante sana kwa mafunzo mazuri
ReplyDeleteHilo jiko linatakiwa liwe na moto??
ReplyDeleteSasa utapikaje bila kuwa na moto ndugu ila uweke moto wa wastani sana
DeleteAsante saanaaa
ReplyDeleteNimeipenda ntajaribu umetupa somo kwasisi ambao hatuna majiko ya ges
ReplyDeleteSafi
ReplyDeletenatka kupiga keki lakin mimi na kilo mmoja ya unga nachangnya vip naomba kujuwa
ReplyDeleteAsanteee kwa mafunzo
ReplyDeleteAsante kwa somo
ReplyDeleteSorry asante kwa mafunzo je maziwa ya mtindi au fresh
ReplyDeleteFresh
DeleteAsantehene nikikosa siag nitumie nn
ReplyDeleteDada .... Safi sana
ReplyDeleteHaiweki amira??
ReplyDeleteviko viwili ni vile vya nusu au robo mala mbili samahani dia
ReplyDeleteNitajalibu kupika
ReplyDeletekeki kuwa kama ugali nini kosa? yaani kutochambuka
ReplyDeleteNimeipika imetoka vizuri sana. Very spongy. Nimetumia jiko la mkaa maana umeme ulikuwa umekatika
ReplyDeleteAsanteh sana Dada samahani ukikosa siagi unawaza tumiaa mafuta ya kupi
ReplyDeletekia???
nimependa maelezo yako ila mm kila nikijaribu keki inapasuka kwa juuuu shida nn
ReplyDeleteUkikosa siagi unatumia mini tujibu tafathali
ReplyDeleteGood lesson, siagi/ blue band ni lazima katika mchanganyiko. Lkn, wakati wa kuioka unaweza paka mafuta ya Kula ya kawaida ktk sufuria
ReplyDeleteWaoooh! Maelezo mazuri. Nimekuwa na kwama kwama ktk pishi hili. Sasa nitakuwa fundi. Khakhaa.... At once niliweka hamira kumbe haitakiwi. Uwiiii. Nilikosa blue band nikatia mafuta yaliyonikuta nilitoa uji mbich sio kek . . . .
ReplyDeleteNi lazima utumie maziwa au kuna mbadala?
ReplyDeleteAhsante saaana naamin nikfanya ntakuwa mjuzi pia
ReplyDeleteKila nikijaribu inatoka kama mkate, shida nini
ReplyDeleteMTU anaeza tumia sufuria ya kawaida
ReplyDeleteSina mayai ya kienyeji
ReplyDeleteasante mm ni bint yak lkn samahan unga vk viwil saw na nus au rob
ReplyDelete