Hakuna kitu chochote kitamu chenye harufu na radha nzuri kama keki uliyoipika kwa mikono yako. Upishi wa keki ni mwepesi sana endapo mpishi atazingatia vitu muhimu vinavyohitajika pamoja na hatua zake. MAHITAJI *unga vikombe2 *maziwa kikombe1 *sukari kikombe1 *siagi kikombe1 *baking powder vijiko vidogo 2 *mayai 6 yakienyeji *vanilla matone mawili au limao 1 Zingatia Limao au vanilla hutumika kwaajili ya kupunguza harufu ya mayai kwenye keki.kwahiyo ukikosa vanilla pia waweza kutumia maganda ya limao. Pia andaa jiko lako la mkaa mapema ili lipate joto pamoja na sufuria iliyopakwa siagi ndani ili kuzuia keki kuganda. HATUA *Andaa bakuli lako la udongo na mwiko ambao utatumia kuchanganya mchanganyiko wako *chukua kikombe kimoja cha siagi na utie katika bakuli pamoja na kikombe kimoja cha sukari. *koroga mchanganyiko wa sukari na siagi mpaka pale utakapolainika na chembe chembe za sukari kupotea kabisa *Weka yai moja baada ya jingine huku ukiendelea kuukoroga mch
Blog hii imelenga kukuhabarisha na kukufahamisha yale yanajiri kila kona ya dunia, na pia kukuburudisha. Hivyo basi hakikisha huachi kutembelea na kuperuzi katika blog hii mara kwa mara. Pia mnakaribishwa kutangaza nasi ili kuifanya blog iwe 'active'ili kuendelea kukuhabarisha bila tatizo, Karibuni.....kwa tangazo wasiliana kwa simu namba 0682 518456
Comments
Post a Comment