Skip to main content

MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI

            Mwanafunzi  wa  mwaka  wa  kwanza  katika   Chuo  Kikuu  cha  Taifa Cha Usafirishaji(NIT), Aquillina  B  Aquillini amepoteza  maisha  katika   vurugu  zilizotokea katika uchaguzi  wa  kinondoni  baada  ya  kupigwa  risasi  na  polisi wakati  wakitawanya  waandamanaji  wa  CHADEMA.
            Kwa  mujibu  wa  Mkuu  wa  chuo hicho,  Zakaria Mnagilwa,  amesema  kwamba mwanafunzi  huyo  aliaga analepeka  barua  ya   maombi ya  mafunzo  ya  kazi  kwa vitendo(Field) na  ndipo  umauti huo  ulipomkuta.
            Baadhi  ya  mastaa  wakubwa  nchini  akiwemo  Diamond Platnumz, Shilole, Jackline Wolper  na  wengine wamesikitishwa  sana  na  tukio  hilo  na  wengi wao  wameandika  maneno  yenye  kuonesha  dhahiri  uchungu  wao  juu  ya  tukio  hilo  kwenye  kurasa  zao  za  mtandao  instagram  na  wengine  wakimuombea  apumzike  kwa  amani  na  kutoa  pole  kwa  familia  ya  marehemu.
  # MtawaOne blog  inatoa  pole  kwa  familia.....PUMZIKA  KWA  AMANI  AQUILLINA.

Comments

Popular posts from this blog

JIFUNZE KUPIKA KEKI KWA JIKO LA MKAA

             Hakuna kitu chochote kitamu chenye harufu na radha nzuri kama keki uliyoipika kwa mikono yako. Upishi wa keki ni mwepesi sana endapo mpishi atazingatia vitu muhimu vinavyohitajika pamoja na hatua zake. MAHITAJI *unga vikombe2 *maziwa kikombe1 *sukari kikombe1 *siagi kikombe1 *baking powder vijiko vidogo 2 *mayai 6 yakienyeji *vanilla matone mawili au limao 1 Zingatia Limao au vanilla hutumika kwaajili ya kupunguza harufu ya mayai kwenye keki.kwahiyo ukikosa vanilla pia waweza kutumia maganda ya limao. Pia andaa jiko lako la mkaa mapema ili lipate joto pamoja na sufuria iliyopakwa siagi ndani ili kuzuia keki kuganda. HATUA *Andaa bakuli lako la udongo na mwiko ambao utatumia kuchanganya mchanganyiko wako *chukua kikombe kimoja cha siagi na utie katika bakuli pamoja na kikombe kimoja cha sukari. *koroga mchanganyiko wa sukari na siagi mpaka pale utakapolainika na chembe chembe za sukari kupotea kabisa *Weka yai moja baada ya jingine huku ukiendelea kuukoroga mch

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI

Vichwa  vikubwa  vya magazeti ya  leo  jumapili

MWINGINE ATEULIWA NA KUPANDISHWA CHEO LEO.

             Raisi wa   Jamuhuri   ya   Muungano wa Tanzajia Mhe.John Pombe Magufuli , amemteua na kumpandisha cheo Bw. Mohamed Hassan Haji, kuwa kamishna wa polisi Zanzibar, kuanzi, leo Feb 10, 2018.                Bw. Mohamed Hassan Haji amepandishwa  cheo kutoka  kuwa  kamishna msaidizi wa jeshi la polisi(ACP)  na kuwa kamishna wa polisi (CP).                  Kamishna  wa polisi  Mohamed Hassan Haji amechukua nafasi iliyoachwa wazi na kamishna wa polisi Hamad Omar Makame ambaye  amestaafu.