Skip to main content

Posts

Showing posts from February, 2018

JIFUNZE KUPIKA KEKI KWA JIKO LA MKAA

             Hakuna kitu chochote kitamu chenye harufu na radha nzuri kama keki uliyoipika kwa mikono yako. Upishi wa keki ni mwepesi sana endapo mpishi atazingatia vitu muhimu vinavyohitajika pamoja na hatua zake. MAHITAJI *unga vikombe2 *maziwa kikombe1 *sukari kikombe1 *siagi kikombe1 *baking powder vijiko vidogo 2 *mayai 6 yakienyeji *vanilla matone mawili au limao 1 Zingatia Limao au vanilla hutumika kwaajili ya kupunguza harufu ya mayai kwenye keki.kwahiyo ukikosa vanilla pia waweza kutumia maganda ya limao. Pia andaa jiko lako la mkaa mapema ili lipate joto pamoja na sufuria iliyopakwa siagi ndani ili kuzuia keki kuganda. HATUA *Andaa bakuli lako la udongo na mwiko ambao utatumia kuchanganya mchanganyiko wako *chukua kikombe kimoja cha siagi na utie katika bakuli pamoja na kikombe kimoja cha sukari. *koroga mchanganyiko wa sukari na siagi mpaka pale utakapolainika na chembe chembe za sukari kupotea kabisa *Weka yai moja baada ya jingine huku ukiendelea kuukoroga mch

RAISI MAGUFULI AMEVITAKA VYOMBO VYA DOLA KUWACHUKULIA HATUA WALIOHUSIKA NA KIFO CHA MWANAFUNZI AKWILLINA

          Rais  wa  Jumuhuri ya  Muungano  wa  Tanzania, Mhe John  Pombe  Magufuli ameviagiza  vyombo  vya  dola  kufanya  uchunguzi  na  kuwachukulia  hatua  wote  walio  husika  na  kifo  cha  mwanafunzi wa  Chuo  Cha  Usafirishaji(NIT) Akwilina  Akwllini.          Na pia  Raisi  Magufuli  amesikitishwa  na  tukio  hilo  na  kutoa  pole  kwa  familia  ya  marehemu  na  wote  walioguswa  na  msiba  huo. RIP AKWILLINA.
Jipatie  kaptula  na  tisheti za  kijanja  kwa  bei  nafuu  kabisa,  Wanapatika  Dar Es Salaam  karibu  na  chuo  kikuu  cha  Dar  Es  Salaam(UDSM). Kwa  mawasiliano  zaidi  piga simu  namba  0718000005  au  0655320024....NYOTE  MNAKARIBISHWA. Price: 28000

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI

Vichwa  vya  Magazeti ya  siku ya  leo.

MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI

            Mwanafunzi  wa  mwaka  wa  kwanza  katika   Chuo  Kikuu  cha  Taifa Cha Usafirishaji(NIT), Aquillina  B  Aquillini amepoteza  maisha  katika   vurugu  zilizotokea katika uchaguzi  wa  kinondoni  baada  ya  kupigwa  risasi  na  polisi wakati  wakitawanya  waandamanaji  wa  CHADEMA.             Kwa  mujibu  wa  Mkuu  wa  chuo hicho,  Zakaria Mnagilwa,  amesema  kwamba mwanafunzi  huyo  aliaga analepeka  barua  ya   maombi ya  mafunzo  ya  kazi  kwa vitendo(Field) na  ndipo  umauti huo  ulipomkuta.             Baadhi  ya  mastaa  wakubwa  nchini  akiwemo  Diamond Platnumz, Shilole, Jackline Wolper  na  wengine wamesikitishwa  sana  na  tukio  hilo  na  wengi wao  wameandika  maneno  yenye  kuonesha  dhahiri  uchungu  wao  juu  ya  tukio  hilo  kwenye  kurasa  zao  za  mtandao  instagram   na  wengine  wakimuombea  apumzike  kwa  amani  na  kutoa  pole  kwa  familia  ya  marehemu.   # MtawaOne blog  inatoa  pole  kwa  familia.....PUMZIKA  KWA  AMANI  AQUILLINA.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI

Habari  kubwa  kwenye  magazeti  ya  leo